Ijumaa, 25 Septemba 2015

MAGUFULI NA IPSOS

Dar es Salaam. Kampuni ya Ipsos jana ilitangaza matokeo ya utafiti wake wa hali ya kisiasa unaoonyesha kuwa mgombea wa CCM, Dk John Magufuli angeshinda kwa asilimia 62 kama Uchaguzi Mkuu ungefanyika Septemba, huku mgombea wa Chadema, Edward Lowassa akipata asilimia 31.

Utafiti huo unaonyesha mgombea wa ACT-Wazalendo, Anna Mghwira angepata asilimia 0.3, wakati asilimia 7 ya waliohojiwa hawakuwa na chaguo, takwimu ambazo zinaonyesha kasoro kwenye matokeo ya jumla ambayo ni asilimia 100.3 badala ya asilimia 100 kama inavyotakiwa katika utafiti.

Utafiti huo, ulioitwa Ipsos Social Political Economic na Cultural Barometer, ulitolewa jana usiku baada ya kuvujishwa tangu asubuhi na baadhi ya watu waliopiga simu ofisi za Mwananchi ambao baadaye waliutuma kwa barua pepe.

Alipopigiwa jana mchana kuulizwa kuhusu kuwapo kwa ripoti ya utafiti huo, meneja wa Ipsos wa Tanzania, Charles Makau alikana kutuma ripoti yoyote ya utafiti kwa vyombo vya habari, lakini wakati tukienda mitamboni alituma ripoti hiyo hiyo, akiomba Mwananchi imtajie jina la aliyeivujisha ili achukue hatua za kisheria.

“Naomba unipe jina lake au e-mail address yake ili nimjue na nichukue hatua,” alisema Makau. “Lakini hatuna uhusiano wowote na chama chochote wala hatuwajui hao watu wa hicho chama waliowatumia ripoti. Kama utanisaidia, nipe jina ili nichukue hatua.”

Ukusanyaji taarifa ulifanyika kati ya Septemba 5 na 22, kuchanganuliwa Septemba 23 na kutolewa jana, lakini Makau alitetea muda huo mfupi wa kuchanganua taarifa akisema ulitosha.

“Kwanza tumechelewa kutoa ripoti kwa sababu tulitaka iwe nzuri, lakini muda huo wa kumaliza kukusanya taarifa na kuzichanganua unatosha kwa kuwa tunafanya kidigitali,” alisema.

Kama ilivyokuwa kwa utafiti wa Twaweza uliotoka mapema wiki hii, Ipsos imetumia watu 1,836 kutoka Tanzania Bara tu, ikifanya mahojiano ya uso kwa uso kwa kutumia lugha ya Kiswahili na Kiingereza


umeme mara kwa mara Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) limetoa ufafanuzi kuhusu  tatizo la kukatika  kwa ume

Dar es Salaam. Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) limetoa ufafanuzi kuhusu  tatizo la kukatika  kwa umeme linaloendelea nchini linatokana na kuongeza taratibu megawati hadi zifikie megawati 335.

Meneja Mahusiano Adrian Severin alipokuwa kwenye uzinduzi wa usambazaji wa waya za umeme kwenye shule ya Msingi ya Msasani B,amesema tatizo la kukatika kwa umeme litaisha Oktoba mwaka huu baada ya bomba la gesi kujaa baa 52.

Severin amesema Septemba 19 mwa huu Tanesco iliwasha mitambo ya Umeme wa gesi asilia megawati 90 huku wakiendelea kuongeza kidogokidogo kufikia 335 ambazo zinatakiwa kutokana na ukubwa wa bomba hilo.

“Tatizo hili la kukatika kwa umeme litakuwa kwenye mikoa ambayo Gridi ya taifa imepita  hivyo  tulianza kuzalisha megawati 90 na tunaendelea kupandisha kiwango taratibu ili kufikia megawati 335 mwishoni mwa Oktoba mwaka huu,”amesema Severn.

Amesema Tanesco wanaendelea  kuongeza kupandisha kiwango taratibu za megawati ili tatizo la kukatika kwa umeme lipungue kwenye mikoa mbalimbali nchini.

Wakati huohuo  Shirika hilo limesambaza nyaya za umeme zenye thamani ya Sh10 milioni kwenye vyumba 18 vya shule ya Msingi Msasani B.

Severin amesema Tanesco linajihusisha na jamii kwa kusaidia kutoa misaada mbalimbali  ya maendeleo ikiwemo  huduma za afya na kugawa madawati katika shule mbalimbali.

Aidha, Afisa Takwimu Geogre Maiga amesema msaada huo wa umeme utaisaidia shule hiyo kusoma kwa kutumia teknolojia ya kisasa kwa kutumia komputa.

“Kama umeme umeingia kwenye shule hii ninaamini kuwa ndio mwanzo wa kupata komputa ambapo wanafunzi wetu wataweza kujifunza somo la Tehama kwa vitendo,”amesema Maiga.

Jumatano, 30 Julai 2014

BREAKING NEWS DIAMOND PLATINUMZ AWASILI NA KUWAPA HI MASHABIKI

MUda mfupi  baada ya kuchukua tuzo
Diamond amewasili nchini kwake akipita ktk mitaa ya BUGURUNI jijini dar akiwaonyesha mashabiki wake tuzo aliyopata (much love to you)

Jumatatu, 28 Julai 2014

EID MUBARAK NA UDAKU NA Z ZE DON

Udaku na z ze don inapenda kuwa ya kwanza kuwatakia EID MUBARAK.

MARUFUKU KUENDESHA MAGARI NCHINI NIGERIA

Jeshi la Nigeria limepiga marufuku utumizi wa magari katika jimbo la Borno
Jeshi la Nigeria limepiga marufuku utumizi wa magari kwa siku tatu katika jimbo la Borno kaskazini mashariki mwa taifa hilo ili kuzuia tishio la wanamgambo wa Boko Haram.

Msemaji wa jeshi amesema kuwa hatua hiyo itazuia utumiaji wa magari kutekeleza mashambulizi ya kujitolea mhanga wakati wa siku kuu ya Eid ul Fitr.

Wakati huohuo kumekuwa na ripoti ambapo mlipuaji wa kujitolea muhanga amewaua watu kadhaa katika mji wa kazkazini wa KANO.


Kundi la Boko Haram limetishia kulipua bomu la gari
Mwandishi wa BBC Tomi Oladipo anasema kuwa Wanajeshi hao waliwashauri waislamu kuhudhuria swala za Eid karibu na viwanja vilivyopo karibu na makaazi yao kwa kuwa kundi hilo lilikuwa linapanga kutekeleza mashambulizi katika viwanja,masoko pamoja na maeneo mengine ya uma wakitumia magari.

Gavana wa Borno Kassim Shetima amesema kuwa anawaonea huruma maelfu ya watu waliolazimika kutumia mda wao mwingi kutembea hadi katika viwanja vya kufanyia salah,lakini akaongezea kuwa hatua hiyo inalenga kuwalinda .


Jeshi la Nigeria limepiga marufuku utumizi wa magari katika jimbo la Borno
Kundi la Boko haram linadaiwa kuiteka miji kadhaa kusini mwa Borno na kuweka bendera zake.

Jeshi la Nigeria hivi majuzi lilikiri kwamba baadhi ya wanajeshi wake walikuwa wanatoroka kutokana na uvamizi wa wanamgambo hao.

Ijumaa, 25 Julai 2014

NDEGE YA ALIGERIA ILIYOPOTEA ,MABAKI YAKE YAPATIKANA

Mabaki ya ndege iliyopotea ikiwa na watu 116 njiani kutoka Burkanafaso kwenda Algers yamepatikana nchini Mali.

Maafisa wa Jeshi wa Burkina faso wamesema ndege hiyo iliyokuwa chini ya shirika la ndege la Algeria imeanguka karibia kilomita 50 kutoka mpaka wa Burkanafaso.

Waongoza ndege walipoteza mawasilino na ndege hiyo muda mfupi baada ya kupata taarifa kutoka kwa Rubani kuwa alikuwa kwenye eneo lenye hali mbaya ya hewa.

Utafutaji wa ndege hiyo umeanzia katika eneo la Gao mpaka Tessalit. Kumekuwepo na hali mbaya ya hewa kwa zaidi ya saa 24. Waziri wa mambo ya nje wa ufaransa, Laurent Fabius amesema inaonekana ndege ilihamishwa mwelekeo kwa sababu ya hali mbaya ya hewa. „Walikuwa wameelekezwa kubadili njia ya kawaida kutoka na mabadiliko ya hali ya hewa.Ndege ilikuwa ikipaa juu ya eneo la Malian. Pamoja na juhudi kubwa , mapaka sasa hakuna dalili za kupatika na kwa ndege hiyo. Pengine ndege imeangua"

Ameongeza kuwa waziri wa ulinzi wa ufaransa alikuwa akisaidia katika utafutaji wa ndege hiyo. "Waziri wa ulinzi wameviruhusu vyombo vyao kwenda kwenye eneo kuitafuta ndege. Majeshi ya Algeria na Umoja wa mataifa wanafanya hivyo pia. Ndege mbili za jeshi la ufaransa zilizopiga kambi Niyame hivi sasa na tangu asubuhi zimekua zikiitafuta ndege hiyo. Majeshi yetu katika eneo hilo ikiwamo vifaa vya matibabu vyote viko tayari"

Hapo awali, waziri mkuu wa Algeria Abdelmalek Sellal alitoa ufafanuzi wa tukio la kuanguka kwa ndege hiyo. "Usiku wa jana kama saa 9 ndege ya Hispania iliyokodiwa na Shirika la Ndege la Algeria ilikuwa katika safari yake kati ya Ouagadougou na Algiers. Ilipoteza mawasiliano na Rada muda huo wa saa tisa usiku dakika 10 tu baada ya kupaa. Mawasiliano ya mwisho ilikuwa na mnara wa kuongozea ndege ulioko Niger na ndege ilikuwa juu ya Gao, kama kilomita 500 kutoka kwenye mpaka wa Algeria. Kulikuwa na abiria 119 wakiwamo wafanyakazi wake. Utafutaji bado unaendelea na tunawasiliana na mamlaka zinazohusika. Waliokuwa kwenye ndege ni raia wa Algeria pamoja na mataifa mengine"

Mamlaka zinazohusika nchini Burkina Faso ambako ndiko ndege ilitokea wameamua kutoa msaada wa kisaikolojia kwa wanafamilia wa wale waliokuwa katika ndege. Baadhi ya ndugu wamefika katika uwanja wa ndege wa Ouagadougou kufuatilia taarifa kuhusu ndugu zao. Baadhi walikuwa na malalamiko "Tuwanataka watuambie kama ndege hiyo imeanguka, kuna walionusurika, au wote wamekufa. Hayo ndio tunayotaka kujua. Tupo kwenye wakati mgumu. Watatu miongoni mwetu, tulitaka kusafiri na dada yetu lakini tuliamua kuahirisha safari katika dakika za mwisho. Hata hivyo dada yetu yeye aliondoka usiku jana." Mwaume mwingine aliyekuwepo kwenye uwanjahuo wa ndege alisema

HATIMAYE DAWA YA UKIMWI YAPATIKANA

Watafiti katika Chuo Kikuu cha Sayansi na Tiba cha Temple, Marekani wamegundua dawa ya kuangamiza Virusi Vya Ukimwi (VVU) ambayo ni ya uhakika zaidi ukilinganisha na zilizowahi kupatikana katika tafiti za awali duniani.

Dawa yao inaweza kutumika kwa tiba ya wanaoishi na VVU na kinga kwa wale ambao bado hawajaambukizwa.

Mmoja wa watafiti hao, Dk Kamel Khalili aliwaambia waandishi wa habari juzi mjini Philadelphia, Marekani kuwa tofauti na utafiti mwingine, wao wamegundua namna ya kukiondoa kirusi kilichoingia kwenye kinasaba (DNA) ndani ya CD4 na kukitoa nje na hatimaye kukiua.

Alisema dawa hiyo inafanya kazi hiyo bila kuathiri seli za mwili wa binadamu.

Dk Khalili alisema ugunduzi wao ni wa hali ya juu zaidi kwa sababu teknolojia ya kutengeneza dawa hiyo ni tofauti na nyingine zilizokwisha kugunduliwa ambazo hazina uwezo wa kupenya ndani ya seli za binadamu, bali kuathiri tu VVU vilivyopo nje yake, ndani ya mfumo wa damu.

“Dawa yetu inakivuta kirusi nje ya seli (CD4) bila kuiathiri seli yenyewe na kukiua. Hivyo dawa hii itatumika kwa muda fulani na kuua virusi vyote mwilini na hakuna haja ya kuitumia wakati wote kama ilivyo dawa ya kufubaza VVU (ARV).”

ARV huangamiza VVU vilivyopo kwenye damu na kuendelea kuviacha hai vile ambavyo tayari vimeingia ndani ya CD4, hivyo kufanya virusi kuzuka upya pindi mwathirika anapoacha kutumia dawa.

Mmoja wa wataalamu katika Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu Kituo cha Mbeya (NIMR-MMRC), Clifford Majani ameuelezea utafiti huo kama mwanga mpya katika teknolojia ya kukabili VVU.

“Kama imepatikana teknolojia ya kukiondoa kirusi ndani ya seli ni hatua nzuri ya kukabili VVU. Hili lilionekana kuwa gumu mwanzoni,” alisema Majani.

Alisema imekuwa vigumu kuua kirusi kikiwa ndani ya seli na hata baadhi ya wanasayansi wamejaribu kutengeneza dawa itakayotambua seli zilizoathirika ili ziuawe lakini hilo likawa gumu.

“Inaweza ikapatikana dawa ya namna hiyo (inayoua seli zilizoathirika) lakini ikawa inaathiri vitu vingine ndani ya mwili.
"Hilo halikubaliki. Kikubwa katika ugunduzi huo ni dawa kuweza kukifuata kirusi kinakojificha na kukiondoa, jambo ambalo dawa nyingi zimeshindwa zikiwamo ARV,” alisema.

Hata hivyo, Majani alisema changamoto ambayo inaweza kujitokeza katika majaribio ya dawa hiyo ni usalama wakati wa matumizi.

“Lazima dawa hiyo ichunguzwe isije ikawa inaathiri viungo vingine pamoja na utendaji wa mwili kwa ujumla. Maana hapo ndipo dawa nyingi zinaposhindwa… Tusubiri tuone hii inaweza kuwa na matumaini zaidi,” alisema Majani.

Mkutano wa Ukimwi
Ugunduzi huo umekuja wakati wanasayansi, waunda sera na wadau wa mapambano ya VVU wakiwa wanatoa kauli za kukata tamaa kwenye mkutano wa Ukimwi unaomalizika kesho huko Melbourne, Australia.

Wanasayansi kadhaa wanaotoka kwenye taasisi kubwa za utafiti za VVU wameweka wazi kuwa tafiti nyingi zilizokuwa na matumaini zimeshindwa kufanya kazi kwa asilimia 100 baada ya dawa zake kufanyiwa majaribio kwa sababu dawa zake zinapotumika, vipimo huonyesha wamepona lakini baada ya muda VVU hurejea upya.

“Kinachoonekana ni kwamba virusi hivi hujificha sehemu fulani ya mwili ili visiathirike na kusubiri mtu aache dawa ili virejee upya kushambulia CD4,” alisema Mkurugenzi wa Taasisi ya Utafiti ya wa Magonjwa ya Kuambukiza na Kinga ya Peter Doherty ya Australia, Profesa Sharon Lewin.

Dawa mpya inavyofanya kazi
Dk Khalili alisema wametengeneza dawa yao kwa protini maalumu ambayo inakata sehemu ya seli iliyoshambuliwa na kirusi cha Ukimwi na kukivuta nje.

Baada ya kukivuta, dawa huachana na seli hiyo na kuiacha ikijitibu yenyewe na kupona kabisa kiasi cha kuendelea na kazi zake za kinga mwilini mwa binadamu bila tatizo.

VVU kwa kawaida hushambulia seli kinga aina ya CD4 na kuzifanya kama kiwanda cha kuzalishia virusi vingine.

Kwa kawaida seli ikishaingiliwa na kirusi, huacha kazi yake ya kinga ya mwili na badala yake kuchukua jukumu la kutengeneza VVU.

“Dawa yetu inafanya kazi kwa haraka, kwa makini na bila kuathiri seli,” alijigamba Dk Khalili.
Alisema tayari imefanyiwa majaribio maabara na kuonekana inafanya kazi vizuri na sasa wamehamishia majaribio kwa wanyama.

Katika maabara, alisema dawa hiyo ilifanyiwa majaribio kwa damu ya binadamu na ikaonyesha kufanya kazi kwa asilimia 100.

Dk Khalili anaamini kwamba majaribio hayo yatawachukua miaka michache... “Lakini tunaamini ni mfumo ambao utaweza kufanya kazi vizuri kwa binadamu.”

Alisema wanachofanya sasa ni kuangalia mfumo ambao utakuwa mzuri zaidi kwa ajili ya tiba ya binadamu.

Kwa namna teknolojia ya dawa hiyo ilivyo, alisema wanaweza kuitumia kwa ajili ya kuwatibu wale ambao tayari wameambukizwa na hata kuwakinga wale ambao siyo waathirika.

Uzuri wa dawa hiyo, pia alisema inaweza kutumiwa na mtu ambaye anatumia ARV pasipo kuingiliana kiutendaji.

Ugunduzi wao ulichapishwa kwenye Jarida la Taifa la Elimu ya Sayansi la National Academy of Science la Marekani na kuonekana kuvuta hisia za wengi.

Hali ya Ukimwi duniani
Akizungumza kwenye mkutano wa Melbourne, Profesa Lewin alisema tafiti za sasa zinaonyesha kuwa karibu watu milioni 14 duniani wanaishi na VVU.

Alisema mamilioni ya watu hao wamekuwa wakisaidiwa kwa kutumia ARV, wakati huu ambao bado hakuna kinga wala tiba, inayoaminika.

Alisema ingawa tafiti nyingi hazijaonyesha matumaini waliotarajia ya kupata kinga na chanjo, bado juhudi zinaendelea ili kuhakikisha wanafikia mahali HIV inakuwa haina nafasi katika mwili wa mwanadamu.

Alisema pamoja na matokeo hasi ambayo yamejitokeza kwenye tafiti nyingi, bado anaamini kwamba ipo siku chanjo na tiba vitapatikana.

Wanasayansi waliohudhuria mkutano huo waliitaka dunia isiogope kutokana na kushindwa kwa baadhi ya tafiti kama ilivyokuwa kwa mtoto wa Jimbo la Mississippi, nchini Marekani ambaye alitangazwa amepona na baadaye virusi vikaibuka upya.
Chanzo: Mwananchi