Ijumaa, 25 Septemba 2015

MAGUFULI NA IPSOS

Dar es Salaam. Kampuni ya Ipsos jana ilitangaza matokeo ya utafiti wake wa hali ya kisiasa unaoonyesha kuwa mgombea wa CCM, Dk John Magufuli angeshinda kwa asilimia 62 kama Uchaguzi Mkuu ungefanyika Septemba, huku mgombea wa Chadema, Edward Lowassa akipata asilimia 31.

Utafiti huo unaonyesha mgombea wa ACT-Wazalendo, Anna Mghwira angepata asilimia 0.3, wakati asilimia 7 ya waliohojiwa hawakuwa na chaguo, takwimu ambazo zinaonyesha kasoro kwenye matokeo ya jumla ambayo ni asilimia 100.3 badala ya asilimia 100 kama inavyotakiwa katika utafiti.

Utafiti huo, ulioitwa Ipsos Social Political Economic na Cultural Barometer, ulitolewa jana usiku baada ya kuvujishwa tangu asubuhi na baadhi ya watu waliopiga simu ofisi za Mwananchi ambao baadaye waliutuma kwa barua pepe.

Alipopigiwa jana mchana kuulizwa kuhusu kuwapo kwa ripoti ya utafiti huo, meneja wa Ipsos wa Tanzania, Charles Makau alikana kutuma ripoti yoyote ya utafiti kwa vyombo vya habari, lakini wakati tukienda mitamboni alituma ripoti hiyo hiyo, akiomba Mwananchi imtajie jina la aliyeivujisha ili achukue hatua za kisheria.

“Naomba unipe jina lake au e-mail address yake ili nimjue na nichukue hatua,” alisema Makau. “Lakini hatuna uhusiano wowote na chama chochote wala hatuwajui hao watu wa hicho chama waliowatumia ripoti. Kama utanisaidia, nipe jina ili nichukue hatua.”

Ukusanyaji taarifa ulifanyika kati ya Septemba 5 na 22, kuchanganuliwa Septemba 23 na kutolewa jana, lakini Makau alitetea muda huo mfupi wa kuchanganua taarifa akisema ulitosha.

“Kwanza tumechelewa kutoa ripoti kwa sababu tulitaka iwe nzuri, lakini muda huo wa kumaliza kukusanya taarifa na kuzichanganua unatosha kwa kuwa tunafanya kidigitali,” alisema.

Kama ilivyokuwa kwa utafiti wa Twaweza uliotoka mapema wiki hii, Ipsos imetumia watu 1,836 kutoka Tanzania Bara tu, ikifanya mahojiano ya uso kwa uso kwa kutumia lugha ya Kiswahili na Kiingereza


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni