Alhamisi, 26 Desemba 2013

TUKIO LA AINA YAKE MTU AFARIKI AKIWA NA KETE TUMBONI(PICHA)




HIZI ndizo kete zinazodaiwa kuwa ni madawa ya kulevya yaliyopatikana katika gari baada ya kupekuliwa kituo kikuu cha polisi.

Maiti ikiwa ndani ya gari yenye namba ya usajili T 887 BSW eneo la chumba cha kuhifadhia maiti cha hospotali kuu ya mkoa wa Morogoro, baada ya gari hilo kukamatwa majira ya saa 7 usiku eneo la Mikumi,likiwa na watu watatu na maiti ya binadamu inayodaiwa kupoteza maisha baada ya kumeza kete hizo za zinazodaiwa kuwa ni madawa ya kulevya na kufariki dunia, 


Maiti ikisafirishwa kutoka Tunduma mkoani Mbeya kwenda Jijini Dar es Salaam.
 MWILI wa marehemu, Khalid Abdul Kitala (47) ambaye ni mfanyabiashara wa Kariakoo jijini Dar es Salaam ukiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti cha hospitali kuu ya mkoa wa Morogoro muda mfupi kabla ya mwili huo kufanyiwa uchunguzi na kukutwa na kete 17 zinazodhaniwa kuwa ni madawa ya kulevya katika tukio la kufasarisha maiti iliyotiliwa shaka na askari polisi Mikumi ambao waliweka mtego kufuatia kupata taarifa za tukio hilo na raia wema na kulinasa gari lililokuwa likitokea Iringa kwenda Dar es Salaam majira ya saa 21:26: HRS jana usiku. PHOTO/MTANDA BLOG.

Katika gari la watuhumiwa lilipekuliwa kwa kina na kupatikana kete 7 na kete 17 na kufanya jumla yake kuwa 24 zilizokamatwa na watuhumiwa wapo chini ya ulinzi katika kituo kikuu cha polisi kwa uchunguzi.


K

DIAMOND AMTAMBULISHA TENA WEMA KAMA MPENZI WAKE JANA



HII ilikuwa jana pale Leaders club kwenye show ya Diamond ambapo Wema Sepetu alipanda kwenye stage na kuongea na mashabiki waliofika kwenye show hiyo.
Kwenye hiyo show Diamond aliuliza,”Mnataka kumjua mchumba wangu”?
Show ilivyoendelea Diamond alitaka kuimba wimbo wa

ukimwona akasema, “Naskia ninayetaka kumuimbia wimbo huu yupo humu humu ndani”.
Wema Sepetu akapanda kwenye stage wakaimba na kucheza wote.



Jumatatu, 23 Desemba 2013

UNYAMA TUNDUMA, MTOTO ACHINJWA, HOUSE GIRL ANYONGWA MPAKA KUFA

Watu wasiojulikana wamewaua watoto wawili,mmoja akiwa ni binti wa kazi wa Diwani wa CCM kata ya Mkingamo wilaya Momba mkoani Mbeya.


Chanzo cha mauaji inasemekana ni dhuluma ya viwanja kwa wananchi wa kawaida.

Habari zaidi zinasema kawadhulumu wananchi viwanja vingi sana,wakati mwingine huuza kiwanja kimoja kwa zaidi ya watu watatu.


Inasemekana hata ukimpeleka mahakamani anakushinda kesi,kifupi ni kuwa mahakama aliiweka mfukoni.

CHANZO: Jamii FORUMS

Jumapili, 22 Desemba 2013

tazama video ya young dee kijukuu


MANJI AFUNGUKA

Mwenyekiti wa klabu ya Young Africans Bw. Yusuf Manji amewaomba wanachama, wapenzi na washabiki wasivunjike moyo kwa matokeo ya jana ya mchezo wa kirafiki dhidi ya ya Simba SC, mechi iliyochezwa katika dimba la Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.

Mwenyekiti wa Yanga Bw.Yusuf Manji akiongea na waandishi wa habari makao makuu ya klabu, kushoto ni makamu mwenyekiti Clement Sanga

Akiongea na waandishi wa habari makao makuu ya klabu ya Yanga makutano ya mitaa wa Twiga/Jangwani Manji amesema anajua wanachama, na wapenzi wameumia sana hakuna aliyefurahishwa na matokeo ya kufungwa mabao 3-1 lakini isiwakatishe tamaa uongozi unafanyia kazi mapungufu yaliyojitokeza.
"Mechi ya jana ilikuwa ni bonanza, ndio maana hapakuwa na timu iliyopata pointi katika mchezo huo zaidi ya kusherehekea, sisi tumepata zawadi ya milion 98 wakati wenzetu Simba SC wamepata milion 1, hivyo zaidi sisi tumeendelea kuimarika kiuchumi zaidi wenzetu wameishia kusherehekea" alisema Manji. 
Aidha amesema wachezaji zaidi ya tisa wa Yanga hawajapata muda wa kupumzika tangu mwezi Novemba baada ya kumalizika kwa mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu kwani walijiungana timu za Taifa na wamekua huko kwa takribani mwezi mzima bila kupumzika tofauti na wenzetu Simba SC ambao hawana wachezaji wengi timu ya Taifa.
Manji pia alisema anawapa hongera timu ya Simba SC kwa kushinda bonanza la jana, amesema mchezo wa jana walicheza vizuri hivyo wanastahili pongezi kwa hilo.
Akijibu maswali ya waandishi wa habari juu ya mapungufu yaliyojitokez katika mchezo wa jana, amesema kamati husika inayafanyia kazi na kwa kuwa yeye anasafiri leo kwenda nje ya nchi  majukumu yote amemkabidhi makamu mwenyekiti Clement Sanga mpaka yeye atakaporejea.

TAZAMA VIDEO MPYA YA DIAMOND NA DAVIDO _MY NUMBER1 REMIX


DIAMOND PLATINUM AKIZINDUA VIDEO YAKE MPYA NA WATOTO YATIMA(PICHA)

PICHA-NILIVYOIYONYESHA KWA MARA YA KWANZA VIDEO YA NUMBER 1 REMIX KWA WATOTO WAISHIO KATIKA MAZINGIRA MAGUMU


Kama nilivyotangulia kusema awali kuwa,hawa
 watoto ndiyo mashabiki wetu wakubwa,na mara 
nyingi hawapati fursa ya
 kuhudhuria maonyesho yetu
 ama kukutana na
 sisi..hivyo kutokana na kuwa awali,video 

ya number 1 version ya
 kwanza niliizndua kwa baadhi ya 
watu special pekee..awamu hii,video ya
 number one remix
 niliyoifanya na 
Davido wa Nigeria..nimeamua kuionyesha kwa
 mara ya kwanza kwa
 watoto waishio katika
 mazingira magumu..usisahau pia kuwa tarehe 25
 mwezi huu.mchana .pale Leaders club nitakuwa
 na tamasha  
special kwa  ajili ya watoto ambao wengi hawapati fursa ya
 kuona maonyesho yetu..na siku hiyo hiyo usiku
 tutakuwa Mwanza..get ready ...




 watoto wakiangalia kwa makini kabisa

 Nikisaini Kitabu cha wageni kabla sijaondoka

SIKILIZA NA DOWNLOAD SIMCO ft LULE _MWISHO