Alhamisi, 26 Desemba 2013

TUKIO LA AINA YAKE MTU AFARIKI AKIWA NA KETE TUMBONI(PICHA)




HIZI ndizo kete zinazodaiwa kuwa ni madawa ya kulevya yaliyopatikana katika gari baada ya kupekuliwa kituo kikuu cha polisi.

Maiti ikiwa ndani ya gari yenye namba ya usajili T 887 BSW eneo la chumba cha kuhifadhia maiti cha hospotali kuu ya mkoa wa Morogoro, baada ya gari hilo kukamatwa majira ya saa 7 usiku eneo la Mikumi,likiwa na watu watatu na maiti ya binadamu inayodaiwa kupoteza maisha baada ya kumeza kete hizo za zinazodaiwa kuwa ni madawa ya kulevya na kufariki dunia, 


Maiti ikisafirishwa kutoka Tunduma mkoani Mbeya kwenda Jijini Dar es Salaam.
 MWILI wa marehemu, Khalid Abdul Kitala (47) ambaye ni mfanyabiashara wa Kariakoo jijini Dar es Salaam ukiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti cha hospitali kuu ya mkoa wa Morogoro muda mfupi kabla ya mwili huo kufanyiwa uchunguzi na kukutwa na kete 17 zinazodhaniwa kuwa ni madawa ya kulevya katika tukio la kufasarisha maiti iliyotiliwa shaka na askari polisi Mikumi ambao waliweka mtego kufuatia kupata taarifa za tukio hilo na raia wema na kulinasa gari lililokuwa likitokea Iringa kwenda Dar es Salaam majira ya saa 21:26: HRS jana usiku. PHOTO/MTANDA BLOG.

Katika gari la watuhumiwa lilipekuliwa kwa kina na kupatikana kete 7 na kete 17 na kufanya jumla yake kuwa 24 zilizokamatwa na watuhumiwa wapo chini ya ulinzi katika kituo kikuu cha polisi kwa uchunguzi.


K

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni