Jumatano, 30 Julai 2014

BREAKING NEWS DIAMOND PLATINUMZ AWASILI NA KUWAPA HI MASHABIKI

MUda mfupi  baada ya kuchukua tuzo
Diamond amewasili nchini kwake akipita ktk mitaa ya BUGURUNI jijini dar akiwaonyesha mashabiki wake tuzo aliyopata (much love to you)

Jumatatu, 28 Julai 2014

EID MUBARAK NA UDAKU NA Z ZE DON

Udaku na z ze don inapenda kuwa ya kwanza kuwatakia EID MUBARAK.

MARUFUKU KUENDESHA MAGARI NCHINI NIGERIA

Jeshi la Nigeria limepiga marufuku utumizi wa magari katika jimbo la Borno
Jeshi la Nigeria limepiga marufuku utumizi wa magari kwa siku tatu katika jimbo la Borno kaskazini mashariki mwa taifa hilo ili kuzuia tishio la wanamgambo wa Boko Haram.

Msemaji wa jeshi amesema kuwa hatua hiyo itazuia utumiaji wa magari kutekeleza mashambulizi ya kujitolea mhanga wakati wa siku kuu ya Eid ul Fitr.

Wakati huohuo kumekuwa na ripoti ambapo mlipuaji wa kujitolea muhanga amewaua watu kadhaa katika mji wa kazkazini wa KANO.


Kundi la Boko Haram limetishia kulipua bomu la gari
Mwandishi wa BBC Tomi Oladipo anasema kuwa Wanajeshi hao waliwashauri waislamu kuhudhuria swala za Eid karibu na viwanja vilivyopo karibu na makaazi yao kwa kuwa kundi hilo lilikuwa linapanga kutekeleza mashambulizi katika viwanja,masoko pamoja na maeneo mengine ya uma wakitumia magari.

Gavana wa Borno Kassim Shetima amesema kuwa anawaonea huruma maelfu ya watu waliolazimika kutumia mda wao mwingi kutembea hadi katika viwanja vya kufanyia salah,lakini akaongezea kuwa hatua hiyo inalenga kuwalinda .


Jeshi la Nigeria limepiga marufuku utumizi wa magari katika jimbo la Borno
Kundi la Boko haram linadaiwa kuiteka miji kadhaa kusini mwa Borno na kuweka bendera zake.

Jeshi la Nigeria hivi majuzi lilikiri kwamba baadhi ya wanajeshi wake walikuwa wanatoroka kutokana na uvamizi wa wanamgambo hao.

Ijumaa, 25 Julai 2014

NDEGE YA ALIGERIA ILIYOPOTEA ,MABAKI YAKE YAPATIKANA

Mabaki ya ndege iliyopotea ikiwa na watu 116 njiani kutoka Burkanafaso kwenda Algers yamepatikana nchini Mali.

Maafisa wa Jeshi wa Burkina faso wamesema ndege hiyo iliyokuwa chini ya shirika la ndege la Algeria imeanguka karibia kilomita 50 kutoka mpaka wa Burkanafaso.

Waongoza ndege walipoteza mawasilino na ndege hiyo muda mfupi baada ya kupata taarifa kutoka kwa Rubani kuwa alikuwa kwenye eneo lenye hali mbaya ya hewa.

Utafutaji wa ndege hiyo umeanzia katika eneo la Gao mpaka Tessalit. Kumekuwepo na hali mbaya ya hewa kwa zaidi ya saa 24. Waziri wa mambo ya nje wa ufaransa, Laurent Fabius amesema inaonekana ndege ilihamishwa mwelekeo kwa sababu ya hali mbaya ya hewa. „Walikuwa wameelekezwa kubadili njia ya kawaida kutoka na mabadiliko ya hali ya hewa.Ndege ilikuwa ikipaa juu ya eneo la Malian. Pamoja na juhudi kubwa , mapaka sasa hakuna dalili za kupatika na kwa ndege hiyo. Pengine ndege imeangua"

Ameongeza kuwa waziri wa ulinzi wa ufaransa alikuwa akisaidia katika utafutaji wa ndege hiyo. "Waziri wa ulinzi wameviruhusu vyombo vyao kwenda kwenye eneo kuitafuta ndege. Majeshi ya Algeria na Umoja wa mataifa wanafanya hivyo pia. Ndege mbili za jeshi la ufaransa zilizopiga kambi Niyame hivi sasa na tangu asubuhi zimekua zikiitafuta ndege hiyo. Majeshi yetu katika eneo hilo ikiwamo vifaa vya matibabu vyote viko tayari"

Hapo awali, waziri mkuu wa Algeria Abdelmalek Sellal alitoa ufafanuzi wa tukio la kuanguka kwa ndege hiyo. "Usiku wa jana kama saa 9 ndege ya Hispania iliyokodiwa na Shirika la Ndege la Algeria ilikuwa katika safari yake kati ya Ouagadougou na Algiers. Ilipoteza mawasiliano na Rada muda huo wa saa tisa usiku dakika 10 tu baada ya kupaa. Mawasiliano ya mwisho ilikuwa na mnara wa kuongozea ndege ulioko Niger na ndege ilikuwa juu ya Gao, kama kilomita 500 kutoka kwenye mpaka wa Algeria. Kulikuwa na abiria 119 wakiwamo wafanyakazi wake. Utafutaji bado unaendelea na tunawasiliana na mamlaka zinazohusika. Waliokuwa kwenye ndege ni raia wa Algeria pamoja na mataifa mengine"

Mamlaka zinazohusika nchini Burkina Faso ambako ndiko ndege ilitokea wameamua kutoa msaada wa kisaikolojia kwa wanafamilia wa wale waliokuwa katika ndege. Baadhi ya ndugu wamefika katika uwanja wa ndege wa Ouagadougou kufuatilia taarifa kuhusu ndugu zao. Baadhi walikuwa na malalamiko "Tuwanataka watuambie kama ndege hiyo imeanguka, kuna walionusurika, au wote wamekufa. Hayo ndio tunayotaka kujua. Tupo kwenye wakati mgumu. Watatu miongoni mwetu, tulitaka kusafiri na dada yetu lakini tuliamua kuahirisha safari katika dakika za mwisho. Hata hivyo dada yetu yeye aliondoka usiku jana." Mwaume mwingine aliyekuwepo kwenye uwanjahuo wa ndege alisema

HATIMAYE DAWA YA UKIMWI YAPATIKANA

Watafiti katika Chuo Kikuu cha Sayansi na Tiba cha Temple, Marekani wamegundua dawa ya kuangamiza Virusi Vya Ukimwi (VVU) ambayo ni ya uhakika zaidi ukilinganisha na zilizowahi kupatikana katika tafiti za awali duniani.

Dawa yao inaweza kutumika kwa tiba ya wanaoishi na VVU na kinga kwa wale ambao bado hawajaambukizwa.

Mmoja wa watafiti hao, Dk Kamel Khalili aliwaambia waandishi wa habari juzi mjini Philadelphia, Marekani kuwa tofauti na utafiti mwingine, wao wamegundua namna ya kukiondoa kirusi kilichoingia kwenye kinasaba (DNA) ndani ya CD4 na kukitoa nje na hatimaye kukiua.

Alisema dawa hiyo inafanya kazi hiyo bila kuathiri seli za mwili wa binadamu.

Dk Khalili alisema ugunduzi wao ni wa hali ya juu zaidi kwa sababu teknolojia ya kutengeneza dawa hiyo ni tofauti na nyingine zilizokwisha kugunduliwa ambazo hazina uwezo wa kupenya ndani ya seli za binadamu, bali kuathiri tu VVU vilivyopo nje yake, ndani ya mfumo wa damu.

“Dawa yetu inakivuta kirusi nje ya seli (CD4) bila kuiathiri seli yenyewe na kukiua. Hivyo dawa hii itatumika kwa muda fulani na kuua virusi vyote mwilini na hakuna haja ya kuitumia wakati wote kama ilivyo dawa ya kufubaza VVU (ARV).”

ARV huangamiza VVU vilivyopo kwenye damu na kuendelea kuviacha hai vile ambavyo tayari vimeingia ndani ya CD4, hivyo kufanya virusi kuzuka upya pindi mwathirika anapoacha kutumia dawa.

Mmoja wa wataalamu katika Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu Kituo cha Mbeya (NIMR-MMRC), Clifford Majani ameuelezea utafiti huo kama mwanga mpya katika teknolojia ya kukabili VVU.

“Kama imepatikana teknolojia ya kukiondoa kirusi ndani ya seli ni hatua nzuri ya kukabili VVU. Hili lilionekana kuwa gumu mwanzoni,” alisema Majani.

Alisema imekuwa vigumu kuua kirusi kikiwa ndani ya seli na hata baadhi ya wanasayansi wamejaribu kutengeneza dawa itakayotambua seli zilizoathirika ili ziuawe lakini hilo likawa gumu.

“Inaweza ikapatikana dawa ya namna hiyo (inayoua seli zilizoathirika) lakini ikawa inaathiri vitu vingine ndani ya mwili.
"Hilo halikubaliki. Kikubwa katika ugunduzi huo ni dawa kuweza kukifuata kirusi kinakojificha na kukiondoa, jambo ambalo dawa nyingi zimeshindwa zikiwamo ARV,” alisema.

Hata hivyo, Majani alisema changamoto ambayo inaweza kujitokeza katika majaribio ya dawa hiyo ni usalama wakati wa matumizi.

“Lazima dawa hiyo ichunguzwe isije ikawa inaathiri viungo vingine pamoja na utendaji wa mwili kwa ujumla. Maana hapo ndipo dawa nyingi zinaposhindwa… Tusubiri tuone hii inaweza kuwa na matumaini zaidi,” alisema Majani.

Mkutano wa Ukimwi
Ugunduzi huo umekuja wakati wanasayansi, waunda sera na wadau wa mapambano ya VVU wakiwa wanatoa kauli za kukata tamaa kwenye mkutano wa Ukimwi unaomalizika kesho huko Melbourne, Australia.

Wanasayansi kadhaa wanaotoka kwenye taasisi kubwa za utafiti za VVU wameweka wazi kuwa tafiti nyingi zilizokuwa na matumaini zimeshindwa kufanya kazi kwa asilimia 100 baada ya dawa zake kufanyiwa majaribio kwa sababu dawa zake zinapotumika, vipimo huonyesha wamepona lakini baada ya muda VVU hurejea upya.

“Kinachoonekana ni kwamba virusi hivi hujificha sehemu fulani ya mwili ili visiathirike na kusubiri mtu aache dawa ili virejee upya kushambulia CD4,” alisema Mkurugenzi wa Taasisi ya Utafiti ya wa Magonjwa ya Kuambukiza na Kinga ya Peter Doherty ya Australia, Profesa Sharon Lewin.

Dawa mpya inavyofanya kazi
Dk Khalili alisema wametengeneza dawa yao kwa protini maalumu ambayo inakata sehemu ya seli iliyoshambuliwa na kirusi cha Ukimwi na kukivuta nje.

Baada ya kukivuta, dawa huachana na seli hiyo na kuiacha ikijitibu yenyewe na kupona kabisa kiasi cha kuendelea na kazi zake za kinga mwilini mwa binadamu bila tatizo.

VVU kwa kawaida hushambulia seli kinga aina ya CD4 na kuzifanya kama kiwanda cha kuzalishia virusi vingine.

Kwa kawaida seli ikishaingiliwa na kirusi, huacha kazi yake ya kinga ya mwili na badala yake kuchukua jukumu la kutengeneza VVU.

“Dawa yetu inafanya kazi kwa haraka, kwa makini na bila kuathiri seli,” alijigamba Dk Khalili.
Alisema tayari imefanyiwa majaribio maabara na kuonekana inafanya kazi vizuri na sasa wamehamishia majaribio kwa wanyama.

Katika maabara, alisema dawa hiyo ilifanyiwa majaribio kwa damu ya binadamu na ikaonyesha kufanya kazi kwa asilimia 100.

Dk Khalili anaamini kwamba majaribio hayo yatawachukua miaka michache... “Lakini tunaamini ni mfumo ambao utaweza kufanya kazi vizuri kwa binadamu.”

Alisema wanachofanya sasa ni kuangalia mfumo ambao utakuwa mzuri zaidi kwa ajili ya tiba ya binadamu.

Kwa namna teknolojia ya dawa hiyo ilivyo, alisema wanaweza kuitumia kwa ajili ya kuwatibu wale ambao tayari wameambukizwa na hata kuwakinga wale ambao siyo waathirika.

Uzuri wa dawa hiyo, pia alisema inaweza kutumiwa na mtu ambaye anatumia ARV pasipo kuingiliana kiutendaji.

Ugunduzi wao ulichapishwa kwenye Jarida la Taifa la Elimu ya Sayansi la National Academy of Science la Marekani na kuonekana kuvuta hisia za wengi.

Hali ya Ukimwi duniani
Akizungumza kwenye mkutano wa Melbourne, Profesa Lewin alisema tafiti za sasa zinaonyesha kuwa karibu watu milioni 14 duniani wanaishi na VVU.

Alisema mamilioni ya watu hao wamekuwa wakisaidiwa kwa kutumia ARV, wakati huu ambao bado hakuna kinga wala tiba, inayoaminika.

Alisema ingawa tafiti nyingi hazijaonyesha matumaini waliotarajia ya kupata kinga na chanjo, bado juhudi zinaendelea ili kuhakikisha wanafikia mahali HIV inakuwa haina nafasi katika mwili wa mwanadamu.

Alisema pamoja na matokeo hasi ambayo yamejitokeza kwenye tafiti nyingi, bado anaamini kwamba ipo siku chanjo na tiba vitapatikana.

Wanasayansi waliohudhuria mkutano huo waliitaka dunia isiogope kutokana na kushindwa kwa baadhi ya tafiti kama ilivyokuwa kwa mtoto wa Jimbo la Mississippi, nchini Marekani ambaye alitangazwa amepona na baadaye virusi vikaibuka upya.
Chanzo: Mwananchi

Jumanne, 22 Julai 2014

MIILI ILIYOTUPWA BUNJU ,NANE RUMANDE


Watu wanane wanashikiliwa na polisi wakiwemo Madaktari kwa tuhuma za kuhusika kwenye tukio l a kutupwa kwa mabaki ya miili ya binadamu jana jioni nje kidogo ya jiji la Dsm

Huku likiendelea na uchunguzi kuhusu tukio hilo,Kamanda wa polisi kanda maalum ya Dar es Salaam Suleiman Kova ametangaza kuundwa kwa jopo la upelelezi kuchunguza tukio hilo, ili kubaini taratibu gani zilikiukwa na kujua aina ya mashtaka itakayowakabili.


Mabaki ya miili iliyotupwa eneo la Bunju Dar es Salaam
Uchunguzi wa awali umebainisha kuwa miili hiyo ilikua katika Taasisi ya mafunzo ya udaktari IMTU kabla ya kukutwa imetupwa eneo la Bunju.

Taasisi hiyo imekiri kwamba mabaki ya miili ilikua katika taasisi hiyo lakini haijatoa maelezo kuhusu kutupwa kwa miili hiyo.

Kamanda Kova amewatoa wasiwasi watanzania kuwa hakuna mauaji yoyote ya kimbari yaliyotokea sehemu yeyote nchini hivyo polisi iachiwe ifanye kazi yake kisha itatoa taarifa hapo baadae.

Jumatatu, 21 Julai 2014

Chadema yajipanga uchaguzi serikali za mitaa

Kauli hiyo imetolewa jana Jijini Dar es Salaam na Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Mhe. Freeman Mbowe wakati akitoa maazimio ya kamati kuu ya chama hicho pamoja na mambo mbalimbali yanayohusu maendeleo ya chama hicho.
Kwa upande Mwingine Mhe.Mbowe akizungumzia mchakato wa katiba mpya amesema viongozi wa umoja wa katiba ya wananchi UKAWA bado wanaendelea na msimamo wao wa kutorejea katika bunge maalum la katiba.
Wakati huo huo, mbunge wa jimbo la Ubungo Mh. John Mnyika ameitaka serikali kupitia Wizara ya Maji kuchukua hatua ya kuwaita wakazi wa Goba jijini Dar es Salaam, kuwaeleza hatma ya kupata maji ili kuepusha hasira walizonazo wananchi hao juu ya ahadi ya kupata maji isiyotimizika.
Akiongea na East Africa Television jijini Dar es Salaam, Mh. Mnyika amesema wakazi wa jiji la Dar es Salaam wanataka uhakika wa kupata maji safi, ambayo imekuwa ni kero yao ya muda mrefu sasa.

UCHAWI CHEMBA WAKWAMISHA MAENDELEO

Baadhi ya wakazi katika wilaya ya Chemba wakitafuta maji
Miradi ya maj
i na umeme katika baadhi ya maeneo ya halmashauri ya wilaya ya Chemba imeshindwa kutekelezeka kutokana na imani za kishirikina ambapo wakandarasi wa umeme wamekuwa wakikumbana na nyoka kila wanapochimba mashimo ya kusimika nguzo, na kwenye miradi ya maji mabomba yanapasuka muda mfupi baada ya kufukiwa ardhini kwa madai ya wakandarasi hao kutowashirikisha wazee wa kimila kabla ya kuanza kwa miradi hiyo.
Changamoto hiyo ya kushangaza kama sio ya kustaajabisha imeibuliwa na mwenyekiti wa halmashauri hiyo mpya Muheshimiwa Rajabu kwenye zoezi la kutia saini mikataba ya ujenzi wa mifumo wa usambazaji maji katika vijiji vitano vya wilaya hiyo ambapo ametoa taadhari kwa wakandarasi watakaotekeleza miradi hiyo kuacha kuchelea kuwaona wazee wa vijiji hivyo ili kuepuka matukio kama hayo kuendelea kujitokeza na kuchelewesha maendeleo kwa wananachi.
Kaimu mhandisi wa maji wawilaya ya Chemba Robert Mganga amethibitisha kuwepo kwa matukio ya aina hiyo na kudai kuwa yamekuwa yakikwamisha utekelezaji wa miradi huku mhandisi kutoka wakala wa umeme vijijini (REA) Onesmo Kilamuhama akidai kuwa wamekuwa wakilazimika kufanya matambiko mara kwa mara na wazee wa kimila ili kupata ridhaa ya kutekeleza mradi huo.
Awali katika zoezi hilo mkuu wa wilaya ya Chemba Francis Isaac Mtinga amesema uhaba wa maji ni changamoto kubwa inayowakabili wakazi wa wilaya hiyo ambapo asilimia 66 hawapati maji kabisa  hali inayochangiwa na kushindwa kushiriki katika shughuli za maendeleo, huku wakikabiliwa na magonjwa yakiwemo ya ngozi, homa ya matumbo na kuhara mara kwa mara.
Ujenzi wa mfumo wa usambazaji maji katika vijiji vitano vya wilaya hiyo kupitia mpango wa serikali wa matokeo makubwa sasa utagharimu kiasi cha zaidi ya shilingi bilioni 1.187 ambao unatarajiwa kupunguza adha ya maji na wananchi kusafiri umbali mrefu kutafuta huduma hiyo huku wakishindwa kushiriki katika shughuli za maendeleo

TZ YASHINDWA KUJITETEA NYUMBANI

Timu ya taifa ya Tanzania "Taifa Stars"
Tanzania ikiwa katika uwanja wake wa nyumbani Taifa Stars imeshindwa kutamba mbele ya majirani zao kutoka kusini Msumbiji baada ya kulazimishwa sare ya bao 2 - 2 katika kuania kucheza michuano kombe la Mataifa ya Afrika.

Wakati Tanzania ikitoka sare na Msumbiji majirani zao Kenya wakiwa Huko Lesotho, wameshindwa kutamba na hivyo wakaambulia kupigwa bao 1 - 0.

Nchi ya Afrika mashariki iliyofurukuta ni Uganda iliyokwamisha 2 - 0 dhidi ya Mauritania. Huko Benin, Malawi imepigwa bao 1 - 0

Bila shaka Wacongo wamekesha wakicheza muziki baada ya kuwavumishia majirani zao Rwanda kwa bao 2 - 0

Sierra Leone nao wakawabamiza ushelisheli bao 2 - 0.

UCHUNGUZI JUU YA NDEGE YA MALAYSIA

Wito zaidi umetolewa kwa wataalamu wa kimataifa waruhusiwe kikamilifu kulikagua eneo ambalo ndege ya Malaysia ilidunguliwa mashariki mwa Ukraine.

Waziri mkuu wa Australia, Tony Abbott, anasema kuwa hakuna usimamizi mzuri katika eneo ambapo ndege ya Malaysia ilianguka wiki iliyopita.

Anasema huenda ni kwa hakika wapiganaji wanaoiunga Urusi mkono waliidunguwa ndege hiyo na jinsi wanavyolidhibiti eneo hilo ni kama kuwa na wahalifu wanaosimamia eneo ambalo uhalifu umefanyika.

Raia 37 wa Ukraine walikuwa miongoni mwa watu 300 waliouawa.

Australia inaunga mkono azimio la Umoja wa mataifa la kutaka wachunguzi waruhusiwe kuingia katika eneo hilo kufanya uchunguzi wa kina.

Haya yakijiri, Rais wa Urusi, Vladimir Putin, amesema kua atafanya kila awezalo, kuhakikisha kuwa mgogoro wa Ukraine unapata ufumbuzi.


Mabaki ya ndege ya Malaysia iliyodunguliwa
Rais Putin alitoa taarifa mapema asubuhi ya leo ambalo lilionekana kwenye mtandao wa ikulu ya Rais.

Tangazo lenyewe ni kinyume na matamshi aliyotaoa wiki jana aliposema kuwa maafisa wa Ukraine ndio wa kulaumiwa kwa kutokea kwa ajali hiyo.

Putin amesema kuwa tukio hilo linapaswa kuungunisha mataifa hayo mawili wala sio kuleta mgawanyiko zaidi ingawa aliongeza kwamba kama makubaliano ya kusitisha vita Ukraine Mashariki yasingevunjika mwezi Juni na mapigano kuanza tena, mkasa huu umgezulika.

Alisema kuwa kila mtu katika eneo hilo ambaye amehusika katika mgogoro huo anapaswa kuwajibika.

Alisema ni muhimu kufanya kila liwezekanalo, kuhakikisha usalama wa wataamu wa kimataifa katika eneo hilo unahakikishwa, ili wataalamu hao waweze kufanya uchunguzi.

Pia ametoa wito wa kuruhusu misaada kuweza kuwafikia waathiri wa wa vita.

JESHI LA ISRAEL LAINGIA GAZA

Jeshi la ardhini la Israel laingia Gaza
NYUMBANI


Sasa Israel yashambulia Gaza wakitumia vikosi vya angani, ardhini na majini
Israel imeanzisha operesheni ya nchi kavu pamoja na mashambulizi ya anga na baharini dhidi ya vuguvugu la kupigania uhuruwa palestina Hamas katika ukanda wa Gaza.
Katika kipindi cha siku kumi zilizopita zaidi ya wapalestina mia mbili wameuwawa katika mashambulizi ya anga yaliyotekelezwa na Israel na Muisraeli mmoja aliuwawa katika mashambulizi ya mizinga ya roketi kutoka Gaza.
Oparesheni hiyo ya kupeleka majeshi ya ardhini imenza usiku, ni operation kubwa kufanywa katika kipindi cha miezi mitano.
Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amesema lengo ni kuharibu kabisa miundo mbinu na silaha zinazotumiwa na vuguvugu la Hamas kuishambulia Israel.
Vifaru karibu kumi vimeshuhudiwa vikielekezwa Gaza huku mashambulio ya angani na majini yakiendelea, ripoti ambazo hazijathibitishwa zinasema huenda hata hospitali zimegwa na mizinga.

Raia wa Gaza walia wakisema hamna pakutorokea huku mashambulizi ya Israel yakiongezeka
Watu zaidi ya 3 wamefariki katika duru hii ya mapigano mbali na wale zaidi ya 200 waliofariki awali.
Kundi la Hamas limesema watajibu oparesheni hiyo vilivyo lakini Israel inasema Hamas watapewa kipigo cha kudumu na kitakachowasambaratisha kabisa.
Israel imewaita maelfu ya wanajeshi wake wa akiba kuweka nguvu zaidi katika operation hiyo.
Jana jamii ya kimataifa ilikuwa na matumaini makubwa kwamba huenda kukawa na usitishwaji mapigano wa kudumu baada pande zote mbili kukubali mapendekezo ya kusitisha mapigano kwa mda wa saa 5 za kuruhusu huduma za kibinadamu.
Mengi ya majumba na Miundo mbinu ya Gaza imebomolewa kwenye mashambulio hayo na maeneo mengi yanakosa hata maji safi ya kunywa.
Vilio na hali ya taharuki imetanda lakini pande zote mbili hazionekani kulegeza misimamo yao.
Huku Wapalestina wakikabiliwa na maisha hayo magumu katika kipindi hiki cha mfungo wa Ramadhan,wengi wa-Israeli waliokaribu na mpaka na Gaza wanaunga mkono operation hiyo, lakini wengine wanahoji gharama ya operation ya ardhini.

Jumatatu, 17 Machi 2014

angalia jinsi ng'ombe wa kichina wanavyopiga


tazama jamaa huyu alivyo ni noma polisi wa kibongo mjipange

MAMIA WAMZIKA MAMA WA MSANII MAARUFU KATIKA FILAMU YA SIRI YA MTUNGI LEO JIJINI DAR, PICHA 40 ZA MATUKIO YA MSIBANI HIZI HAPA

Daudi Michael ( Duma )  kushoto mwenye suti nyeusi msanii maarufu aliyefunika katika Filamu iitwayo SIRI YA MTUNGI leo amemzika mama yake mzazi baada ya kumuuguza kwa
mda mrefu kidogo hatimaye kufariki dunia jana.
Kushoto ni Msanii aliyefiwa na mama yake mzazi, Hapo pichani amekumbatiana na msanii mwenzie maarufu kutoka bongo movie's Shija katika hali ya kuliwazana kusahau yaliopita maana yote ni mipango ya mungu haipingiki hata kidogo..

Mtu wa karibu wa msanii huyo aliyeondokewa na mama yake mzazi aliiambia Website ya Masai Nyotambofu wasanii walionyesha ushirikiano wa hali ya juu kwa kuhudhuria katika msiba huo na huo ndio mfano mzuri kwa wasanii tupendane wakati wa raha na wakati wa matatizo pia. M/mungu ailaze roho ya marehemu mahala pema peponi.
Kupa, Kitale Teja na Mkono wa mkonole wakiwa katika hali ya majonzi kufuatia msiba huo..


Mwanadada Sheri Mwana kushoto anaumwa lakini alihudhuria msiba huo.


Shija akiwa makaburini..




Taswira ya msibani nyumbani kwa kina Daudi Michael ( Duma ).








Majanja, Kupa na Shija..


Majanja akipiga menyu










Mwili wa marehemu ukiwa kwenye gari tayari kupelekwa makaburini kuhifadhiwa..



Baadhi ya wasanii wakiwa makaburini katika hali ya majozi


Mchaga akiuzunika hapo..





Msanii mkongwe 'Mtitu' akitoa maelekezo ya ratiba ya mazishi.

Hapo ndipo alipolala l