Ijumaa, 25 Septemba 2015

MAGUFULI NA IPSOS

Dar es Salaam. Kampuni ya Ipsos jana ilitangaza matokeo ya utafiti wake wa hali ya kisiasa unaoonyesha kuwa mgombea wa CCM, Dk John Magufuli angeshinda kwa asilimia 62 kama Uchaguzi Mkuu ungefanyika Septemba, huku mgombea wa Chadema, Edward Lowassa akipata asilimia 31.

Utafiti huo unaonyesha mgombea wa ACT-Wazalendo, Anna Mghwira angepata asilimia 0.3, wakati asilimia 7 ya waliohojiwa hawakuwa na chaguo, takwimu ambazo zinaonyesha kasoro kwenye matokeo ya jumla ambayo ni asilimia 100.3 badala ya asilimia 100 kama inavyotakiwa katika utafiti.

Utafiti huo, ulioitwa Ipsos Social Political Economic na Cultural Barometer, ulitolewa jana usiku baada ya kuvujishwa tangu asubuhi na baadhi ya watu waliopiga simu ofisi za Mwananchi ambao baadaye waliutuma kwa barua pepe.

Alipopigiwa jana mchana kuulizwa kuhusu kuwapo kwa ripoti ya utafiti huo, meneja wa Ipsos wa Tanzania, Charles Makau alikana kutuma ripoti yoyote ya utafiti kwa vyombo vya habari, lakini wakati tukienda mitamboni alituma ripoti hiyo hiyo, akiomba Mwananchi imtajie jina la aliyeivujisha ili achukue hatua za kisheria.

“Naomba unipe jina lake au e-mail address yake ili nimjue na nichukue hatua,” alisema Makau. “Lakini hatuna uhusiano wowote na chama chochote wala hatuwajui hao watu wa hicho chama waliowatumia ripoti. Kama utanisaidia, nipe jina ili nichukue hatua.”

Ukusanyaji taarifa ulifanyika kati ya Septemba 5 na 22, kuchanganuliwa Septemba 23 na kutolewa jana, lakini Makau alitetea muda huo mfupi wa kuchanganua taarifa akisema ulitosha.

“Kwanza tumechelewa kutoa ripoti kwa sababu tulitaka iwe nzuri, lakini muda huo wa kumaliza kukusanya taarifa na kuzichanganua unatosha kwa kuwa tunafanya kidigitali,” alisema.

Kama ilivyokuwa kwa utafiti wa Twaweza uliotoka mapema wiki hii, Ipsos imetumia watu 1,836 kutoka Tanzania Bara tu, ikifanya mahojiano ya uso kwa uso kwa kutumia lugha ya Kiswahili na Kiingereza


umeme mara kwa mara Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) limetoa ufafanuzi kuhusu  tatizo la kukatika  kwa ume

Dar es Salaam. Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) limetoa ufafanuzi kuhusu  tatizo la kukatika  kwa umeme linaloendelea nchini linatokana na kuongeza taratibu megawati hadi zifikie megawati 335.

Meneja Mahusiano Adrian Severin alipokuwa kwenye uzinduzi wa usambazaji wa waya za umeme kwenye shule ya Msingi ya Msasani B,amesema tatizo la kukatika kwa umeme litaisha Oktoba mwaka huu baada ya bomba la gesi kujaa baa 52.

Severin amesema Septemba 19 mwa huu Tanesco iliwasha mitambo ya Umeme wa gesi asilia megawati 90 huku wakiendelea kuongeza kidogokidogo kufikia 335 ambazo zinatakiwa kutokana na ukubwa wa bomba hilo.

“Tatizo hili la kukatika kwa umeme litakuwa kwenye mikoa ambayo Gridi ya taifa imepita  hivyo  tulianza kuzalisha megawati 90 na tunaendelea kupandisha kiwango taratibu ili kufikia megawati 335 mwishoni mwa Oktoba mwaka huu,”amesema Severn.

Amesema Tanesco wanaendelea  kuongeza kupandisha kiwango taratibu za megawati ili tatizo la kukatika kwa umeme lipungue kwenye mikoa mbalimbali nchini.

Wakati huohuo  Shirika hilo limesambaza nyaya za umeme zenye thamani ya Sh10 milioni kwenye vyumba 18 vya shule ya Msingi Msasani B.

Severin amesema Tanesco linajihusisha na jamii kwa kusaidia kutoa misaada mbalimbali  ya maendeleo ikiwemo  huduma za afya na kugawa madawati katika shule mbalimbali.

Aidha, Afisa Takwimu Geogre Maiga amesema msaada huo wa umeme utaisaidia shule hiyo kusoma kwa kutumia teknolojia ya kisasa kwa kutumia komputa.

“Kama umeme umeingia kwenye shule hii ninaamini kuwa ndio mwanzo wa kupata komputa ambapo wanafunzi wetu wataweza kujifunza somo la Tehama kwa vitendo,”amesema Maiga.